Friday, April 20, 2018

Matip ndo bye bye hadi msimu ujao

Jurgen Klopp amepigilia mstari baada ya kuthibitisha kuwa beki Joel Matip hatopatikana hadi mwishoni mwa msimu kutokana na kukabiliwa na majeraha.

" Kitu kirahisi nachoweza kusema  ni kwamba Matip (Joel) hatutakuwa nae tena katika michezo iliyobaki, ila nachofahamu tutaanza nae msimu akiwa kamili kabisa," Klopp

Klopp amtakia kila la heri Wenger

 Mjerumani Jurgen Klopp ameshindwa kuficha hisia zake baada ya kusikia taarifa za kung'atuka kwenye klabu ya Arsenal kwa Kocha wake Mfaransa Arsene Wenger mwishoni mwa msimu huu.

Gerrard kuchukua mikoba ya Klopp?

Mchezaji mwenye heshima zaidi katika kikosi cha Liverpool katika karne hii ya 21, Steven Gerrard ametoa tathimini yake ya mwaka wa kwanza kwenye maisha yake mapya ya ukocha akisema amepata changamoto kubwa ambayo imezidi kumjenga.

Liverpool, Napoli kukipiga nchini Ireland

Kwa mujibu wa gazeti la Independent Sport, Liverpool inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki kujiandaa na msimu dhidi ya wakali kutoka nchini Italia, Napoli.

Henderson afunguka kuhusu wachezaji wenzake

Kepteni Jordan Henderson amesema ilikuwa changamoto kubwa kwake kukaa jukwaani kuutazama mchezo wa pili wa robo fainali ya UEFA dhidi ya Manchester City na kuwapongeza wachezaji wenzake kwa kupigana kiume na kufuzu.

Robertson atabiriwa makubwa na Dalglish

Legend mwenye heshima kubwa katika uwanja wa Anfield, King Kenny Dalglish ameweka wazi mapenzi yake kwa beki wa kushoto, Andy Robertson akisema kuwa ni mmoja wa mabeki bora na usajili bora kufanywa na Klopp msimu huu.

Lovren, Gomez kuwakabili West Brom kesho?

Liverpool kesho inakabiliwa na mchezo mgumu kwenye Ligi Kuu EPL wakati ambapo itakua wageni wa 'wabishi' West Bromwich Albion . Kumbuka WBA ndio walioitoa Liverpool kwenye kombe la FA.