Saturday, September 17, 2016

JE WAJUA:SIRI ILOYOPO KATI YA USHINDI WA KLOPP DHIDI YA KLABU KUBWA


Kwa taarifa yako tu,Kocha wa Liverpool,Jurgen Klopp ni kocha wa mechi kubwa ambapo ameweza kupata matokeo katika mechi zote kubwa ambazo ameiongoza Liverpool kwa msimu wa 2015/16 na hata msimu huu pia wa 2016/17 .

Hata hivyo katika mahojiano na LiverpooolFc Tv ,Klopp amefichua kuwa sababu kubwa ambayo imekuwa ikichangia kikosi chake kupata matokeo katika mechi kubwa ni pamoja na morali ya hali ya juu ambayo wachezaji wake wanakuwa nayo.

Amesema kuwa pamoja na hayo,pia maandalizi anayoyafanya na hamasa wanayowapa wachezaji wake huchangia kuamsha hali ya kujituma na kuhakikisha timu inapata matokeo.

Hata hivyo Klopp ameweka wazi pia hofu ya kufungwa na klabu kubwa huongezeka maradufu pale wanapowafikiria mashabiki zao,hali inayopelekea kuwaambia wachezaji wake kupambana ili kuwapa mashabiki furaha.

Chini ni baadhi ya Rekodi ambazo zinadhihirisha jinsi ambavyo Klopp ameweza kuvitingisha timu vigogo vya ligi kuu ya Uingereza.

  • 17/10/15 - Tottenham (a) DREW 0-0
  • 21/11/15 - Man City (a) WON 4-1
  • 26/12/15 - Leicester (h) WON 1-0
  • 13/01/16 - Arsenal (h) DREW 3-3
  • 02/02/16 - Leicester (a) LOST 0-2
  • 02/03/16 - Man City (h) WON 3-0
  • 02/04/16 - Tottenham (h) DREW 1-1
  • 14/08/16 - Arsenal (a) WON 4-3
  • 27/08/16 - Tottenham (a) DREW 1-1
  • 10/09/16 - Leicester (h) WON 4-1

No comments:

Post a Comment