Saturday, September 17, 2016

NANI KAMA JURGEN KLOPP,AICHAPA CHELSEA MBELE YA ABRAMOVICH


NANI kama Jurgen Klopp? Kocha huyo wa Liverpool jioni hii amefanikiwa kuiadhibu Chelsea kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu England iliyopigwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.


Dejan Lovren alikuwa wa kwanza kumfurahisha Klopp katika dakika ya 17 alipoiandikia Liverpool bao la kwanza akineemeka na pande la Philippe Coutinho.

Dakika ya 36, Jordan Henderson naye akafanya yake alipoandika bao la pili la Liverpool na kuifanya timu hiyo iende mapumziko ikiwa kifua mbele.

Juhudi za Diego Costa zilizaa matunda dakika ya 61 alipoitumia vizuri pasi ya Nemanja Matic na kuipatia Chelsea bao la kufutia machozi.

Timu hizo zote sasa zina pointi 10 katika mechi tano ingawa Chelsea ni ya tatu ikineemeka na mabao machache ya kufungwa wakati Liverpool ni ya nne.

No comments:

Post a Comment